Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 02:26

Russia yaondolewa kwenye baraza la haki za binadamu la UN


Baraza la umoja wa mataifa, New York. PICHA: AFP
Baraza la umoja wa mataifa, New York. PICHA: AFP

Baraza kuu la umoja wa mataifa limepiga kura na kuiondoa Russia kutoka kwa baraza la haki za binadamu, kufuatia ukandamizaji wa haki za binadamu kwa kuvamia Ukraine kivita.

Nchi 93 zimeunga mkono kura hiyo, 24 zikapinga na 58 kujizuia kupiga kura.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield, ameambia waandishi wa habari kwamba hawataruhusu Russia kuendelea na ukandamizaji na ukiukaji wa haki za kibinadamu, huku ikidai kwamba inaheshimu haki za kibinadamu.

Russia imeonya kwamba kura ya kuindoa kwenye baraza hilo ni hatua isiyo ya kirafiki, itakayokuja na athari zake za ushirikiano.

Kura hiyo imepigwa baada ya Ukraine kushutumu Russia kwa mauaji ya mamia ya raia katika mji wa Bucha, Ukraine.

Russia inakuwa nchi ya pili kuondolewa kwenye baraza la haki za kibinadamu la umoja wa mataif abaada ya Libya iliyoondolewa mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG