Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 02:26

Kura dhidi ya Russia kufanyika leo UN


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia baraza la usalama la umoja mataifa lenye makao yake makuu New York, kwa njia ya video, April 5, 2022. PICHA: AP
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia baraza la usalama la umoja mataifa lenye makao yake makuu New York, kwa njia ya video, April 5, 2022. PICHA: AP

Baraza kuu la umoja wa mataifa linatarajiwa kupiga kura hii leo ya kuiondoa Russia kutoka katika baraza la haki za binadamu, kufuatia ukiukaji mkubwa sana wa haki za binadamu kwa kuivamia Ukraine kivita.

Theluthi mbili ya kura za wanachama zinahitajika ili kuiondoa Russia katika baraza hilo.

Wanadiplomasia wa nchi za magharibi wana Imani kwamba kura hiyo itafaulu.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield, amewaambia waandishi wa habari kwamba hawataruhusu Russia kuendelea na ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu, huku ikidai kwamba inaheshimu haki za binadamu.

Russia imeonya kwamba kura ya kuiondoa kwenye baraza hilo itaonekana kuwa hatua isiyo ya kirafiki, itakayokuja na athari zake za ushirikiano.

Marekani imetangaza kwamba inataka Russia kuondolewa kwenye baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa baada ya Ukraine kuishutumu Russia kwa mauaji ya mamia ya raia katika mji wa Bucha, Ukraine.

Russia imekanusha ripoti za kuua raia nchini Ukraine.

XS
SM
MD
LG