Maandamano yaliyoidhinishwa na serikali dhidi ya kampeni ya kijeshi ya Israeli huko Ukanda wa Gaza yalifanyika katika maeneo kadhaa ya mji wa Cairo na maeneo mengine ya Misri siku ya Ijumaa.
Hata hivyo, baadhi ya waandamanaji mjini Cairo walitembea hadi Tahrir Square - kitovu cha uasi wa Misri wa 2011 - ambao haukuwa miongoni mwa maeneo yaliyoidhinishwa kwa maandamano yanayowaunga mkono Wapalestina.
Waandamanaji hao walitawanywa haraka na maafisa wa usalama.
Maandamano ya umma ambayo hayajaidhinishwa yamepigwa marufuku nchini Misri na Tahrir Square, ambayo ilitengezezwa upya miaka kadhaa iliyopita, Tahrir Square inafuatiliwa sana na huduma za usalama kwa sababu ya umaarufu wake.
"Takriban watu 40 kati ya waliokamatwa walikuwa Cairo, 65 wakiwa Alexandria, na wengine wachache kutoka mikoa mingine.
Kumi na wanne kati ya waliowekwa kizuizini kutoka Cairo walifikishwa kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma," wakili wa haki za binadamu Nabeh Elganadi alisema.
Takriban wafungwa 18 kutoka Cairo waliachiliwa siku ya Jumatatu "na idadi hiyo huenda ikaongezeka," aliongeza.
Maafisa wa mahakama na msemaji wa wizara ya mambo ya ndani hakuweza kupatikana mara moja kwa maoni.
Baadhi ya taarifa za habari hii zilitoka shirika la habari la AFP.
Forum