Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:33

Wakili Kenya aitaka mahakama kumfungulia Jenerali Muhoozi mashtaka ya uhaini


Jenerali wa Jeshi la Uganda Muhoozi Kainerugaba
Jenerali wa Jeshi la Uganda Muhoozi Kainerugaba

Wakili mmoja nchini Kenya amewasilisha malalamiko akiitaka mahakama itoe amri ya kumuita mahakamani Jenerali wa Jeshi la Uganda Muhoozi Kainerugaba kujibu shutuma za kosa  la uhaini kutkana na matamshi  yake ya kuutaka kutuma jeshi kuivamia Nairobi.

Bw Apollo Mboya, Mkuu wa zamani wa Chama cha Mawakili Kenya, katika ombi alilowasilisha katika mahakama ya hakimu mkazi ya Milimani, Nairobi, pia anataka amri itolewe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) na Inspekta Jenerali wa Polisi Kenya kuwasilisha mahakamani repoti ya uchunguzi na karatasi ya mashtaka, iwapo ipo, kuhusiana na kosa hili linalodaiwa.

Kama DPP hataki kufanya hivyo au atashindwa kumfungilia mashtaka na kumshtaki mkuu wa jeshi la nchi jirani katika kipindi cha siku 14, Bw Mboya anataka apewe mamlaka na mahakama kuanzisha mashtaka binafsi dhidi ya Jenerali Muhoozi kutokana na matamshi yake ya karibuni kwenye Twitter akitishia kuanzisha uvamizi wa kijeshi kuikamata Nairobi.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma wa Kenya, Noordin Haji, Nairobi, Kenya July 23, 2019. REUTERS/Stringer
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma wa Kenya, Noordin Haji, Nairobi, Kenya July 23, 2019. REUTERS/Stringer

“Hali ya kutochukua hatua yoyote kwa upande wa DPP na IGP siyo tu inahatarisha usalama wa taifa wa Jamhuri ya Kenya lakini pia ni kinyume na thamini za kitaifa za uzalendo unaoelezwa katika kifungu cha 10 cha Katiba ya nchi,” alisema Bw Mboya.

Wakili huyo anaamini kuwa Jenerali Muhoozi, ambaye pia ni mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amefanya makosa ya uhaini kulingana na ujumbe wa tweet zake zenye utata.

Anadai kuwa makosa yanayoshutumiuwa ni tishio kwa heshima ya mipaka ya Kenya.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la The East African linalochapishwa Kenya.

XS
SM
MD
LG