Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:39

Brigedia Muhoozi aapishwa rasmi kuwa Meja Jenerali wa jeshi la Uganda


Meja Jenerali,Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Meja Jenerali,Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Mkuu wa kikosi maalum cha uongozi katika jeshi la Uganda, Brigedia Muhoozi Kainerugaba ameapishwa rasmi katika nafasi ya Meja Jenerali wakati wa sherehe ambazo zilifanyika katika wizara ya ulinzi katika mji mkuu Kampala.

Kikosi maalum cha uongozi kinahusika kumlinda rais pamoja na mafuta na taasisi nyingine nchini humo. Kainerugaba ambaye ni mtoto wa kwanza wa kiume wa Rais Yoweri Museveni alipandishwa cheo pamoja na maafisa wengine.

Kupandishwa kwake cheo kumechochea shutuma kwenye mitandao ya kijamii nchini uganda huku wakosoaji wakidai kuwa ni sehemu ya mpango wa Rais Museveni kutaka kumsimika mtoto wake kuwa mrithi wake. Jenerali muasi katika jeshi, David Sejusa, mratibu wa zamani wa idara za upelelezi za Uganda katika ofisi ya rais alitoa shutuma hizo alipozungumza na Sauti ya Amerika-VOA.

Jenerali David Sejusa akiwa kizimbani kusikiliza kesi yake.
Jenerali David Sejusa akiwa kizimbani kusikiliza kesi yake.

Sejusa ametaka uchunguzi ufanywe. Alisema mpango huo unahusisha njama za kuua maafisa waandamizi wa utawala ambao wanapinga mpango wa mrithi wa bwana Museveni.

Wakosoaji wanasema kupanda haraka cheo kwa Muhoozi Kainerugaba katika nafasi ya kamanda wa kikosi maalum cha jeshi katika UPDF ni aina fulani ya mpango wa urithi. Serikali imekanusha kuwepo kwa mpango kama huo.

Katika mahojiano na VOA, Meja Chris Magezui, msemaji wa kikosi maalum cha jeshi alisema shutuma hizo hazina ukweli wowote. “ukosoaji huo hauna msingi. Na unabainisha siasa za ndani zilivyo nchini. Ni kwa vile Muhoozi Kainerugaba ni mtoto wa rais basi asiangaliwa kwa juhudi zake kama mtu binafsi, nia yake ya dhati kulitumikia jeshi”.

Magezui amekanusha ripoti za vyombo vya habari vya ndani kwamba kikosi hicho kinafanya maamuzi yake mbali na UPDF.

Alisema huo ni upotoshaji wa habari, ambao umefanywa kwa makusudi na baadhi ya watu, na hilo si sahihi hata kidogo. Kikosi maalum cha jeshi ni moja ya vikosi ndani ya UPDF. Kumekuwepo na majadiliano na uongozi wa jeshi kupanua kikosi hicho maalum kuwa ni idara ya tatu ambapo inamaanisha kuwa UPDF itakuwa na idara tatu, ambazo zinajumuisha jeshi la anga, jeshi la ardhini na kikosi maalum alisema magezi.

XS
SM
MD
LG