Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 08:26

Waasi wazidi kusonga mbele na kuingia mashariki mwa DRC


Wanajeshi wa FARDC wakipambana na M23 huko Lubero, jimbo la Kivu Kaskazini, DRC Oktoba 27, 2024. REUTER.
Wanajeshi wa FARDC wakipambana na M23 huko Lubero, jimbo la Kivu Kaskazini, DRC Oktoba 27, 2024. REUTER.

Mashariki mwa DRC bado inaendelea kukumbwa na vitendo vya ghasia zinazofanywa na waasi na sasa wakiwa wameingia katika mji wa Butembo na kwingineko ambako tayari wameteka vijiji zaidi ya 10.

Inaonekana kuwa waasi wanazidi kusonga mbele hatua ambayo inaliweka jeshi la FARDC kupungukiwa nguvu ya kupambana nao.

Ingawa walinda amani wa SADC na MONUSCO wako katika maeneo ya DRC lakini hali ya uasi bado inaongezeka.

Wakati huo huo, wakulima wengi wanaokwenda shambani mashariki mwa DRC wanalindwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umekuwa chini ya uangalizi mkubwa kwa miaka mingi huku mzozo mashariki mwa nchi baina ya makundi ya uasi, na vikosi vya ulinzi na wanamgambo wengine ukiendelea.

Katika Kijiji cha Dhendro, wakulima wameonyesha uungaji mkono wa mkubwa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani – MONUSCO.

Wakulima hao wengi walihama kutoka kwenye nyumba zao kutokana na mzozo huo, wengi waliokoseshwa makazi kutokana na mzozo huo na sasa wanajificha katika kambi katika na kambi ya Umoja wa Mataifa.

MONUSCO imepelekwa Congo tangu mwaka 2010 wakati ilipochukua udhibiti kutoka kwenye operesheni za awali za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kulinda eneo la mashariki lenye mzozo mkubwa linalopakana na Rwanda.

Baadhi ya taarifa hii inatoka shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG