Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 16, 2024 Local time: 03:27

Mazungumzo mapya ya kumaliza ghasia mashariki mwa DRC kufanyika Angola wikiendi


Kutoka kushoto: Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Angola João Lourenço na Rais Felix Tshisekedi.
Kutoka kushoto: Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Angola João Lourenço na Rais Felix Tshisekedi.

Marais wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watakutana Angola siku ya Jumapili kwa ajili ya mazungumzo mapya yanayolenga kumaliza ghasia mashariki mwa DRC.

Tangu kuibuka tena mwaka 2021 kwa wanamgambo wa M23 wanaoungwa mkono na Kigali, wanaodai kutetea Watutsi wameteka maeneo mengi ya DRC , kuwakosesha makazi maelfu ya watu na kusababisha mgogoro mbaya wa kibinadamu.

Mapema mwezi Agosti , Angola ilisimamia mashauriano tete ya sitisho la mapigano ambayo yalipelekea utulivu katika mstari wa

mbele lakini pande zote mbili ziliendelea kushambuliana na mapigano yameongezeka tangu mwishoni mwa Oktoba.

Rais wa Angola Joao Lourenco aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika kama mpatanishi , ameonyesha matumaini hapo jana kwamba mkutano utakaofanyika Luanda unaweza kupelekea makubaliano ya amani.

Kigali imethibitisha kwamba rais wa Rwanda Paul Kagame atahudhuria mkutano wa jumapili akifuatana na Waziri wake wa Mambo ya Nje Olivier Nduhungirehe .

Forum

XS
SM
MD
LG