Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:09

Makombora ya Israel yaua watu 16 wakiwemo watoto, wanawake


Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas
Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas

Maafisa wa Palestina wamesema kwamba makombora ya Israel kusini na katikati mwa Gaza yameua watu 16 wakiwemo watoto watatu na wanawake watano.

Idadi kubwa ya vifo vilitokana na mashambulizi yalikuwa katika mji wa kusini wa Khan Younis ambao umeshuhudia mashambulizi mazito katika muda wa zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Miili ya waliouawa mehifadhiwa katika hospitali ya Nasser.

Mwandishi wa shirika la habari la Associated press amehesabu miili ya waliofariki ikiwemo watu wa familia moja waliofariki baada ya nyumba yao kupigwa na kushambuliwa katika sehemu ya Fakhari, mashariki mwa Khan Younis.

Shambulizi jingine lilipiga nyumba Battn al-Samin, kusini mwa Khan Younis na kuua watu watano wakiwemo wanawake wawili.

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amekutana na mwana mfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman leo Jumatano kabla ya kuhitimisha ziara yake ya ghafla na kurudi ukingo wa magharibi.

Abbas amesema kwamba alihitimisha ziara yake ya ghafla nchini Saudi Arabia na kurudi ukingo wa magharibu kutokana na mashambulizi makali na ya kiwango kikubwa yanayotekelezwa na jeshi la Israel.

Maafisa wa Palestina wamesema kwamba wanajeshi wa Israel wamewaua Wapalestina tisa na kufunga njia zote za kuingia mji wa Jenin.

Israel imekuwa ikitekeleza kile imekitaja kama operesheni ya kijeshi karibu kila siku katika ukingo wa magharibi, tangu Oktoba 7, wanamgambo wa Hamas walipofanyanya shambulizi kutokea Gaza na kusababisha vita vikali vinavyoendelea.

Israel imesema kwamba operesheni yake ya kijeshi ina lengo la kuwamaliza nguvu wanamgambo wa Hamas na kuzuia mashambulizi dhidi ya raia wake.

Forum

XS
SM
MD
LG