Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:53

Jeshi la Israel lamuokoa mateka aliyekuwa anashikiliwa na Hamas tangu Oktoba 7


Mateka aliyeokolewa na jeshi la Israel Qaid Farhan Alkadi, akipewa matibabu hospitalini, Agosti 27, 2024.
Mateka aliyeokolewa na jeshi la Israel Qaid Farhan Alkadi, akipewa matibabu hospitalini, Agosti 27, 2024.

Israel Jumanne ilisema ilimuokoa mateka mwingine kati ya mateka 250 waliotekwa nyara na wanamgambo wa Hamas wakati wa shambulizi lao baya la mwezi Oktoba.

Jeshi la Israel lilisema lilimpata Qaid Farhan Alkadi mwenye umri wa miaka 52, wakati wa “operesheni tete katika Ukanda wa kusini wa Gaza” huku mapigano yakipamba moto katika vita vya miezi 10 na nusu.

Jeshi lilisema aliokolewa kutoka kwenye handaki lakini halikutoa maelezo zaidi.

Alkadi alitambulishwa kama Muyahudi kutoka jamii ya Kiarabu ya walio wachache ya Bedouin, ambaye alikuwa anafanya kazi kama mlinzi kwenye kiwanda cha kupakia bidhaa huko Kibbutz Magen, moja ya jamii kadhaa za wakulima ambazo zilishambuliwa tarehe 7 Oktoba. Ana wake wawili na ni baba wa watoto 11.

Forum

XS
SM
MD
LG