Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 01:54

Israel yatoa chanjo za polio kwa zaidi ya watu milioni 1 huko Gaza


Wapalestina wapiga foleni kuchota maji huko Deir al-Balah, katika Ukanda wa Gaza, Juni 20, 2024. Picha ya AP
Wapalestina wapiga foleni kuchota maji huko Deir al-Balah, katika Ukanda wa Gaza, Juni 20, 2024. Picha ya AP

Jeshi la Israel Jumapili lilisema chanjo za polio zilitolewa huko Gaza kwa zaidi ya watu milioni 1, baada ya kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa katika eneo hilo katika kipindi cha robo karne.

Haikufahamishwa wazi jinsi zaidi ya chanjo hizo 25,000 zitasambazwa huko Gaza, ambako mapigano na mzozo unaoendelea ulikwamisha juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu wakati wa vita vya zaidi ya miezi 10.

Visa vingine vya polio vinashukiwa katika eneo lilihobaribiwa sana baada ya virusi hivyo kugunduliwa kwenye maji machafu katika maeneo sita tofauti mwezi Julai.

Makundi ya misaada yanapanga kuwachanja zaidi ya watoto 600,000 wenye umri ulio chini ya miaka 10 na yameomba vita visitishwe kwa haraka ili kutoa chanjo nyingi.

Shirika la afya duniani(WHO) na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) yalisema, sitisho la mapigano kwa angalau siku saba linahitajika.

Umoja wa Mataifa una lengo la kuleta dozi milioni 1.6 za chanjo ya polio ndani ya Gaza, ambako maelfu ya Wapalestina waliohamishwa kwenye makazi yao wanasongamana ndani ya kambi za mahema ambazo hazina maji safi au mfumo sahihi wa kusindika maji taka na takataka nyingine.

Familia wakati mwingine hutumia maji machafu kunywa au kusafisha vyombo.

Forum

XS
SM
MD
LG