Majeshi ya Israel yalifanya mashambulizi ya anga leo Jumatano katika eneo linalokaliwa kimabavu huko ukingo wa Magharibi na kusababisha vifo vya watu tisa.
Jeshi la Israel limeripoti kufanya operesheni za kukabiliana na ugaidi katika mji wa Jenin, Tulkarm na eneo la kambi ya wakimbizi ya Al-Far'a na kuwaua jumla ya wanamgambo tisa.
Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina limesema limesafirisha miili ya watu tisa kutoka maeneo hayo, pamoja na watu wengine 13 waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo ya Israel.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz amesema kwenye mtandao wa X leo Jumatano kwamba Israel lazima ishughulikie kitisho cha ugaidi katika Ukingo wa Magharibi kama ilivyo katika Ukanda wa Gaza, na kuishutumu Iran kwa kufadhili na kuwapa silaha wanamgambo katika Ukingo wa Magharibi.
Forum