Kitendo cha kupuuzia kutekeleza hatua hiyo imepelekea ECOWAS kuonya kuwa inaweza kusababisha uingiliaji kati wa kijeshi.
ECOWAS, imesema itatoa taarifa kwa hatua zinazofuata, kuujibu utawala wa kijeshi kukataa kutekeleza maagizo ifikapo Jumapili iliyopita, kama nchi za kigeni zenye nguvu zinavyosema zinatarajia kuwepo na suluhu ya amani.
ECOWAS imechukua msimamo mgumu wakati wa mapinduzi yaliyofanyika Julai 26 ikiwa ni ya saba katika eneo hilo katika kipindi cha miaka mitatu.
Licha ya kwamba nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa uranium na mafuta na nafasi yake katika vita vya wanamgambo wenye msimamo mkali wa kiislamu, Niger inashikilia nafasi muhimu ya kimkakati kwa ajili ya Marekani, Ulaya, China na Russia.
Forum