Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:49

Ufaransa yaahidi kuunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa kiraia Niger


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Ufaransa ilisema Jumamosi itaunga mkono juhudi za kurejesha uongozi wa kiraia nchini Niger kufuatia mapinduzi ya kijeshi, siku moja baada ya jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kusema kuwa una mpango wa kuingilia kijeshi.

Mapinduzi ya kijeshi ya Niger, ambayo ni ya saba katika Afrika Magharibi na Kati katika kipindi cha miaka mitatu, yametikisa eneo la Sahel magharibi, Niger ikiwa mojawapo ya mataifa maskini zaidi duniani yenye umuhimu wa kimkakati kwa mataifa yenye nguvu duniani.

Wakuu wa Ulinzi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wananuia kuchukua hatua za kijeshi ikiwa viongozi wa mapinduzi hawatamrejesha madarakani Rais aliyechaguliwa Mohamed Bazoum ifikapo Jumapili, na hivyo kuzua hali ya mzozo zaidi katika eneo ambalo tayari linapigana na uasi wa wapiganaji wa Kiislamu.

Kiongozi wa mapinduzi mwenye umri wa miaka 59, Jenerali Abdourahamane Tiani, ambaye alipata baadhi ya mafunzo yake ya kijeshi nchini Ufaransa, alisema jeshi halitarudi nyuma.

"Ufaransa inaunga mkono kwa uthabiti na azma juhudi za ECOWAS kushinda jaribio hili la mapinduzi," wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilisema katika taarifa yake baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Catherine Colonna kukutana na Waziri Mkuu wa Niger Ouhoumoudou Mahamadou mjini Paris.

Forum

XS
SM
MD
LG