Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:13

Rais Biden aagiza kuachiliwa mara moja Rais wa Niger Bazoum


Biden
Biden

Biden alisema katika taarifa yake kuwa Niger “inakabiliwa na changamoto kubwa kwa demokrasia yake.”

“Wananchi wa Niger wanahaki ya kuchagua viongozi wao. Wameeleza matakwa yao kupitia uchaguzi huru na haki – na hilo lazima liheshimiwe,” alisema Biden.

Wakuu wa ulinzi kutoka Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi walikuwa wanatarajiwa kukamilisha siku ya pili ya mazungumzo katika nchi jirani ya Nigeria kuhusu hali ilivyo huko.

Siku kadhaa baada ya mapinduzi, ECOWAS iliweka vikwazo dhidi ya viongozi wa mapinduzi hayo na kupanga siku ya Jumapili kikomo cha mapinduzi hayo na Bazoum arejeshwe madarakani huku kukiwa na uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi kama hatarejeshwa mamlakani.

Jenerali Abdourahamane Tchiani, ambaye alijitangaza kuwa mkuu mpya wa nchi, alisema katika hotuba yake kupitia televisheni Jumatano kuwa wanajeshi waliofanya mapinduzi “wanapinga kwa ujumla vikwazo hivyo na wanakataa kusalimu amri kwa vitisho vyovyote, kokote vinakotokea. Tunapinga uingiliaji kati wowote wa masuala ya ndani ya Niger.

Abdel-Fatau Musah, kamishna wamasuala ya siasa, amani na usalama wa ECOWAS amewaambia waandishi wa habari Jumatano mjini Abuja kuwa hatua ya kijeshi itakuwa “njia ya mwisho” ya jumuiya hiyo ya Afrika Magharibi. Lakini Musah alisema maandalizi yanatakiwa yafanyike kwa uwezekano huo.

“Kuna haja ya kuonyesha kuwa siyo tu tunapiga kelele lakini pia tunaweza kuuma,” alisema.

ECOWAS pia ilituma ujumbe Jumatano huko mji mkuu wa Niger, Niamey, kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa kijeshi.

Uingereza ilisema siku ya Alhamisi ilikuwa inapunguza kwa muda wafanyakazi katika ubalozi wake mjini Naimey kutokana na wasi wasi wa kiusalama.

Siku ya Jumatano, Marekani ilisema imeamuru “kuondoka kwa muda kwa wafanyakazi wasio muhimu wa serikali ya Marekani na wanafamilia wanaostahiki kufanya hivyo kutoka Ubalozi wa Marekani mjini Niamey.” Pia imeongeza tahadhari yake ya kusafiri kwa kiwango cha 4 – Usisafiri – kwa ajili ya Niger.

Chanzo cha habari hii inatokana na taarifa za mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG