Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:01

Kiongozi wa mapinduzi nchini Niger apinga shinikizo la kurejesha utawala kwa Rais Bazoum


Kiongozi wa mapindunzi nchini Niger Jenerali Abdourahamane Tiani
Kiongozi wa mapindunzi nchini Niger Jenerali Abdourahamane Tiani

Kiongozi wa mapinduzi nchini Niger Jumatano amesema utawala wa kijeshi hautatishwa na shinikizo la kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum, na hivyo kuzidisha mvutano na Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika magharibi (ECOWAS).

Katika hotuba kwa njia ya televisheni, Abdourahamane Tiani amesema utawala wa kijeshi “unapinga vikwazo hivi kabisa na unakataa kusalimu amri kwa vitisho vyovyote, popote vinapotoka. Tunakataa uingiliaji kati wa aina yoyote katika masuala ya ndani ya Niger.

ECOWAS imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kudhibiti kudorora kwa demokrasia katika eneo la Afrika magharibi na iliapa kwamba mapinduzi ya kijeshi hayatavumiliwa tena baada ya wanajeshi kuchukua madaraka katika nchi wanachama wa ECOWAS, Mali, Burkina Faso na Guinea na jaribio la mapinduzi nchini Guinea-Bissau katika miaka miwili iliyopita.

Forum

XS
SM
MD
LG