Niger ilifunga anga yake siku ya Jumapili hadi itakapotoa taarifa baadaye, ikielezea tishio la kuingiliwa kijeshi kutoka jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi baada ya viongozi wa mapinduzi kukataa amri ya kumrejesha madarakani rais wa nchi hiyo aliyepinduliwa.
Awali, maelfu ya wafuasi wa utawala wa kijeshi walimiminika kwenye uwanja wa michezo mjini Niamey katika mji mkuu, wakishangilia uamuzi wa kutosalimu amri shinikizo kutoka nje kutimiza maagizo ifikapo Jumapili kufuatia unyakuaji madaraka wa Julai 26.
Mapinduzi hayo ambayo ni ya saba huko Afrika Magharibi na Kati katika kipindi cha miaka mitatu, yamelitikisa eneo la Sahel mojawapo ya taifa maskini sana duniani. Kwa kuzingatia utajiri wake wa uranium na mafuta na jukumu lake kuu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu, Niger ina umuhimu kwa Marekani, Ulaya, China na Russia.
Wakuu wa Jeshi wa Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) wamekubaliana uwezekano wa mpango wa hatua za kijeshi, ikiwa ni pamoja na lini na wapi pa kushambulia ikiwa rais aliyekamatwa Mohamed Bazoum hataachiliwa na kurejeshwa madarakani kwa muda uliopangwa.
Forum