Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:34

Utulivu waripotiwa mjini Niamey huku tishio la ECOWAS kutuma wanajeshi Niger likipingwa


PICHA YA MAKTABA: General Abdourahmane Tiani akutana na mawaziri wake.
PICHA YA MAKTABA: General Abdourahmane Tiani akutana na mawaziri wake.

Tarehe ya mwisho iliyowekwa na jumuiya ya ukanda wa Afrika Magharibi, ECOWAS, kwa utawala wa kijeshi wa Niger kumrejesha madarakani rais aliyepinduliwa wa nchi hiyo, ilifika Jumapili.

Hata hivyo, jumuiya hiyo ya kieneo, ambayo imetishia kuingilia kijeshi inakabiliwa na shinikizo kubwa la kutafuta njia za amani zaidi kutatua mzozo huo.

Tarehe ya mwisho iliyowekwa na jumuiya ya ukanda wa Afrika Magharibi, ECOWAS, kwa utawala wa kijeshi wa Niger kumrejesha madarakani rais aliyepinduliwa wa nchi hiyo, ilifika leo Jumapili, lakini jumuiya hiyo ya kikanda, ambayo imetishia kuingilia kijeshi inakabiliwa na shinikizo kubwa la kutafuta njia za amani zaidi.

Shirika la habari la Reuters liliripoti Jumapili kwamba hali ilikuwa tulivu katika mji mkuu wa Niger, Niamey, huku wananchi wakionekana kwendelea na shughuli zao za kawaida.

Baraza la Seneti katika nchi jirani ya Nigeria siku ya Jumamosi lilipinga mpango huo, ikimtaka rais Bola Tinubu, mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo, kutafuta njia nyingine tofauti na utumiaji nguvu. ECOWAS bado inaweza kusonga mbele, kwani maamuzi ya mwisho yanachukuliwa kwa makubaliano na nchi wanachama, lakini onyo la usiku wa kuamkia Jumapili lilizua maswali juu ya hatima ya mpango wake wa kuingilia kati.

Tishio la kuingilia kijeshi lilikuja kufuatia mapinduzi ya Julai 26 wakati wanajeshi walioasi walipomweka kiongozi wao, Jenerali Abdourahmane Tchiani, kama mkuu mpya wa serikali ya Niger. Huku Tchiani akiomba uungwaji mkono wa kitaifa na kimataifa, hofu iliongezeka kwamba mzozo wa kisiasa wa nchi hiyo unaweza kuzuia mapambano yake dhidi ya wanajihadi na kuongeza ushawishi wa Russia katika ukanda wa Afrika Magharibi.

Mapinduzi hayo yanaongeza safu nyingine ya utata katika eneo la Afrika Magharibi ambalo limeshuhudia msururu wa mapinduzi ya kijeshi, itikadi kali za Kiislamu na mabadiliko ya baadhi ya mataifa kuelekea Russia na kundi la mamluki la Wagner.

Forum

XS
SM
MD
LG