Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:00
VOA Direct Packages

Vatican: Hayati Papa Benedict azikwa katika eneo la St. Peter


Ibada ya mazishi ya hayati Papa Benedict, Vatican, Italia.
Ibada ya mazishi ya hayati Papa Benedict, Vatican, Italia.

Baba Mtakatifu Francis aliwaongoza  maelfu ya waombolezaji waliohudhuria ibada maalum ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa kanisa Katoriki, papa  Benedict, iliyofanyika katika eneo la St. Peter.  Papa Francis amemfananisha kiongozi  huyo  na Yesu.

Sauti za kengele zilisikika, watu kumi na mbili walibeba jeneza lililotengenezwa kwa mbao, likiwa na mwili wa papa Benedict kabla ya mazishi yatakayofanyika katika kanisa kubwa kuliko yote huko Christendom.

Makofi yalisikika pande zote, zilizojaa umati mkubwa wa watu, hii ni dalili ya heshima kubwa kwa papa Benedict. Shujaa wa waumini wa kanisa katoliki aliyeishangaza dunia katika uongozi wake wa karibu muongo mmoja pale alipotangaza kujiuzuu upapa.

Akiongoza ibada hiyo ya mazishi , Francis alinukuu maandishi ya biblia na maandiko ya kanisa ambayo yalionyesha kumlinganisha Benedict na Yesu, yakiwemo maneno yake ya mwisho kabla ya kifo chake msalabani: “baba, mikononi mwako, naiweka roho yangu”

Papa Francis pia alitumia maandiko mengine ya biblia alimfananisha Benedict na Yesu yakiwemo “upendo maana yake kuwa yuko tayari kuteseka” na waumini waliitikia “tunamuweka nduyu yetu mikononi mwako bwana”

Ibada hiyo ya mazishi ya Benedict iliyohudhuriwa na makadinali 125, maaskofu 200 na wachungaji wapatao 3,700. Francis alizungumzia “busara, huruma na unyenyekevu uliouonyesha kwa miaka mingi”.

Amemtaja Benedict kwa jina lake mara moja tu, katika mstari wa mwisho aliposema, “ Benedict, rafiki mwaminifu wa Yesu, furaha itimie wakati utapapoisikia sauti yake , sasa na milele” .

Ibada hiyo ya mazishi iliendela mpaka jioni pia ilihudhuriwa na maelfu ya waumini ikiwajumuisha watumishi wa kanisa kutoka nchi mbalimbali duniani na baadhi ya wakuu wachache wa nchi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG