Viongozi mbali mbali kutoka kote ulimwengumi wamekusanyika mjini humo huku maafisa wa usalama wakiwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha usalama .
Takriban watu laki moja wanakadiriwa kuhudhuria mazishi hayo kinyume na watu 60,000 kama ilivyokisiwa awali, kulingana na vyombo vya habari vya Italy.
Zaidi ya watu laki mbili wametoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo katika siku tatu za maombolezo zilizotengwa za kuutazama mwili wake kwenye kanisa la St Peter’s Basilica.
Ujerumani na Italy ndiyo mataifa pekee yalioalikwa rasmi , wakati viongozi kutoka mataifa mengine wakialikwa kibinafsi.