Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:07

Utalii washamiri zaidi Kenya


Watalii wakitembea kando kando ya ufukwe wa bahari ya Hindi, huku wavuvi wakisukuma mtumbwi wao Januari 18,2016. Picha na REUTERS/Joseph Okanga.
Watalii wakitembea kando kando ya ufukwe wa bahari ya Hindi, huku wavuvi wakisukuma mtumbwi wao Januari 18,2016. Picha na REUTERS/Joseph Okanga.

Kenya ni moja ya nchi  ya Afrika Mashariki ambayo sekta  yake ya  utalii ndiyo  chanzo kikuu cha fedha. Wakati janga la COVID lilipopungua mwaka 2022, ongezeko la fedha  liliongezeka kwa asilimia 83 na kufikia  dola bilioni 2.13.

Wageni waliongezeka kwa asilimia 72 ya kiwango cha kabla ya janga kutokea mwaka 2019. Waziri wa Utalii Peninah Malonza aliwaambia waandishi wa habari, kiwango hicho kimezipita nchi nyingine barani Afrika ambazo zimebaki katika kiwango cha ukuaji wa asilimia 65 kabla ya janga la COVID.

Kenya inatoa safari za kwenye fukwe zake zilizoko ukanda wa pwani wa bahari ya Hindi na maeneo ya ndani ya kwenye mbuga. Malonza alisema Marekani ilikuwa chanzo kikuu cha wageni katika kipindi cha mwaka 2022. Kenya inafuatiwa na Uganda, Uingereza na Tanzania.

Mapato ya utalii yalitabiriwa kuongezeka mpaka dola 3.37 mwaka huu, alisema David Gitonga, mtendaji mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Utalii inayomilikiwa na serikali, ambapo mapato yanatarajiwa kuongezeka na kufikia dola 4.25 mwaka 2027.

Lakini sekta hiyo pia inakabiliwa na changamoto kubwa , alisema Kareke Mbiuki, mwenyekiti wa kamati ya utalii na wanyamapori katika bunge, akielezea kupunguzwa kwa miundombinu inayohitajika na sekta hiyo ikiwa ni moja ya mpango mkubwa wa serikali wa kubana matumizi. Nchi hiyo pia inakabiliwa na ukame uliokithiri, alisema waziri wa utalii, Malonza.

Chanzo cha habari hii ni shirika la Habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG