Wanajeshi wa serikali wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa kundi la ukombozi la Tigray, TPLF tangu tarehe 4 Novemba.
Umoja wa Mataifa unasema kwamba dola za Marekani milioni 25 kati ya msaada huo zitatumiwa kununua dawa kwa ajili ya waliojeruihiwa na wagonjwa pamoja na chakula na maji ya kunywa.
Pia dola milioni 10 zilizobaki zitatumika katika kujenga makazi ya muda, vituo vya afya na visima vya maji kwa ajili ya maelfu ya wakimbizi waliokimbia na kuingia nchi jirani ya Sudan.
Mratibu wa idara ya huduma za dharura ya Umoja wa Mataifa Mark Lowcock anasema migogoro ya aina hii ni vigumu kusitisha pale inapokuwa tabu kudhibiti na hivyo inazusha matatizo makubwa kwa maisha ya watu kwa muda mrefu.