Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:11

Waziri mkuu wa Sudan afanya ziara ya muda mfupi Addis Ababa


Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, aliowasili mjini Addis Ababa, Ethiopia, Dec. 13, 2020. (Twitter - @SudanPMHamdok)
Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, aliowasili mjini Addis Ababa, Ethiopia, Dec. 13, 2020. (Twitter - @SudanPMHamdok)

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alifanya ziara ya muda mfupi Addis Ababa siku ya Jumapili kwa mazungumzo juu ya eneo lenye vita la Tigray nchini Ethiopia, ambako mapigano yamesababisha maelfu ya watu kukimbilia Sudan.

“Ninatarajia kuwa na majadiliano yenye tija juu ya mambo ya kisiasa, kibinadamu na usalama yanayohusu mustakabali wa amani, utulivu na ustawi kwa mataifa yetu mawili yenye udugu na kanda nzima,” Hamdok aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter mapema katika ziara yake.

Ziara ya Hamdok hapo awali ilipangwa kudumu kwa siku mbili, lakini alirudi Sudan baada ya saa chache. Haikujulikana kwa nini safari hiyo ilikatishwa.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema ghasia huko Tigray zimekoma na kwamba hakuna haja ya ombi la Sudan la kusuluhisha mzozo huo.

Tigray, iliyo mkoa wa kaskazini zaidi miongoni mwa majimbo tisa ya Ethiopia, kwa ukaidi walifanya uchaguzi mnamo mwezi Septemba ambapo Debre-tsion Gebre-michael aliibuka mshindi, licha ya uamuzi wa Waziri Mkuu Abiy kuahirisha uchaguzi huo, kutokana na janga la corona.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG