Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:13

Waziri mkuu Abiy atembelea Tigray, msako dhidi ya wapiganaji unaendelea


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Waziri mkuu wa Ethiopia amefanya ziara ya kushtukiza katika mji mkuu wa Mekele, ulio eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia.

Abiy Ahmed ametembelea sehemu hiyo siku moja kabla ya kuanza tena shughuli za kawaida na biashara, ilivyotangazwa na utawala wa mda wa eneo la Tigray.

Abiy amefanya mazungumzo na makamanda wa jeshi walioongoza oparesheni ya kijeshi katika eneo hilo mwezi Novemba baada ya vikosi vya Tigray kushambulia kambi ya jeshi eneo hilo.

Viongozi wa vikosi vya Tigray na makamanda wake wanatafutwa kwa lengo la kufunguliwa mashtaka ya uhalifu na kutaka kupindua serikali.

Kulingana na shirika la habari linalomilikiwa na serikali, Abiy amesisitiza kwamba serikali yake itajenga upya eneo la Tigray na kuendelea kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu wa eneo hilo.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, amesema kwamba amekubaliana na mwenzake wa Ethiopia Abiy Ahmed, kuandaa mkutano wa dharura utakaoleta Pamoja nchi zote za Afrika mashariki ili kujadili namna ya kusuluhisha mzozo wa Tigray nchini Ethiopia.

Hadi tukiandaa ripoti hii, serikali ya Ethiopia ilikuwa haijatoa taarifa yoyote kuhusu pendekezo la Hamdok.

Hamdok alitembelea Addis Ababa baada ya idadi ya wakimbizi wanaokimbia Ethiopia na kuingia Sudan wakikimbia vita vya Tigray, kufikia watu 50,000

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG