Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 12:30

Ukraine: Zelenskyy atangaza kufanya mabadiliko katika serikali yake


Naibu mkuu wa ofisi ya Zelenskyy, Kyrylo Tymoshenko awasilisha barua ya kujiuzulu.
Naibu mkuu wa ofisi ya Zelenskyy, Kyrylo Tymoshenko awasilisha barua ya kujiuzulu.

Maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa Ukraine wametangaza kujiuzulu Jumanne katikati ya kile alichosema Rais Volodymyr Zelenskyy kutakuwa na  baadhi ya mabadiliko kikazi katika serikali yake.

Naibu Waziri wa Ulinzi Viacheslav Shapovalov, ambaye alikuwa anasimamia mipango ya kiufundi kwa majeshi ya Ukraine, alijiuzulu wadhifa wake, akieleza madai kuhusu ununuzi wa chakula kashfa ambayo ameikanusha.

Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu Oleksiy Symonenko na naibu mkuu wa ofisi ya Zelenskyy, Kyrylo Tymoshenko, pia walijiuzulu bila ya kutoa sababu za kuachia madaraka.

“Tayari kuna maamuzi ya utumishi – baadhi leo, baadhi kesho – kuhusu maafisa katika ngazi mbalimbali kwenye wizara na miundo ya serikali kuu, na pia katika mikoa na jeshi la polisi,” Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya Jumatatu jioni.

Vifaru vya Ujerumani

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius alisema Jumanne uamuzi wa serikali yake iwapo waidhinishe vifaru vilivyotengenezwa Ujerumani aina ya Leopard 2 utatolewa muda si mrefu.

Akizungumza akiwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg baada ya mazungumzo mjini Berlin, Pistorius aliwaambia waandishi kwamba tathmini inayoendelea inajumuisha kukagua idadi ya vifaru vilivyopo Ujerumani na kufikiria iwapo vinaendana na mazingira ya Ukraine.

Vifaru aina ya Leopard 2 vinavyo tengenezwa Ujerumani.
Vifaru aina ya Leopard 2 vinavyo tengenezwa Ujerumani.

Akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa washirika, ikiwemo wale wanaomiliki vifaru vya Leopard ambavyo wanataka kuvituma Ukraine, Pistorius alisisitiza kuna mshikamano ndani ya NATO na alisema kuwa wakati baadhi ya nchi zinataka kuchukua hatua za haraka kuliko wengine, hawajagawanyika.

"Suluhisho" Litapatikana Hivi Karibuni

Stoltenberg alisema mashauriano kati ya washirika juu ya suala la vifaru yataendelea na kuwa “suluhisho “ litapatikana hivi karibuni.

Aliupokea ujumbe wa Ujerumani kwa washirika kwamba kama wana vifaru vya Leopard na wanataka kuvitayarisha na kutoa mafunzo kwa majeshi ya Ukraine kuvitumia, nchi hizo zinahimizwa kuanza kufanya hivyo.

“Katika kipindi hiki muhimu cha vita, ni lazima tutoe mifumo yenye nguvu na ya kisasa kwa Ukraine, lazima tufanye hivyo kwa haraka,” Stoltenberg alisema.

Aliongezea kuwa kuwapatia vifaru vya kivita majeshi ya Ukraine ni muhimu ili waweze kuyazuia majeshi ya Russia kusonga mbele na kuisaidia Ukraine kukamata tena ardhi yake.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG