Kauli hiyo imetolewa licha ya Ujerumani na Marekani hadi sasa kuonekana kama zinasusia kusambaza vifaa hivyo vya mapigano.
Katika taarifa ya pamoja, Waziri wa Mambo ya Nje Dmytro Kuleba na Waziri wa Ulinzi Oleksii Reznikov walitoa shukrani kwa nchi 50 ambazo zimesaidia kuimarisha ulinzi wa Ukraine.
Pamoja na hayo walisema jeshi la Russia lina faida kubwa ya kiwango cha wanajeshi, na silaha za kijeshi.
Maafisa hao wa Ukraine walisema moja ya mahitaji ya dharura katika kukabiliana na uvamizi wa Russia ulioanza takriban mwaka mmoja uliopita ni kuipatia Ukraine magari ya kisasa ya kivita na kuwapa wanajeshi wa Ukraine uwezo bora wa kurusha na kuendesha vifaru vya Magharibi.