Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 16:01

Ukraine: Mazungumzo ya awali ya maafisa wa Marekani na Russia yatoa matumaini kufanyika mashauriano


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kushoto) na Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergey Shoygu
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kushoto) na Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergey Shoygu

Maafisa wa  juu wa ulinzi wa  Marekani na Russia wamezungumza kwa simu Ijumaa ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa,  wakati maafisa wa Russia wakionyesha dalili mpya za uwazi kuhusu  uwezekano wa kufanyika mashauriano.

Wakati huo huo majeshi ya Ukraine tayari yamepiga hatua kuukaribia mji wa bandari wa kusini wa Kherson unaokaliwa kimabavu na Russia.

Marekani na Russia wote wametoa maelezo ya mazungumzo ya simu hayo kati ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergey Shoygu, wakikiri kuwa lengo la mazungumzo yao lilikuwa vita vya Ukraine.

Kulingana na nyaraka za Pentagon, Austin “ alisisitiza umuhimu wa kuendeleza mawasiliano wakati vita vinaendelea dhidi ya Ukraine.”

Kremlin ilieleza kuwa maafisa hao wawili “walijadiliana matatizo ya usalama wa kimataifa, na hususan hali nchini Ukraine.”

Kabla ya mazungumzo ya simu ya Ijumaa, mara ya mwisho Austin na Shoygu walizungumza ilikuwa Mei 13, wakati Waziri wa Ulinzi wa Marekani alipotoa wito kusitishwa haraka kwa mapigano nchini Ukraine.

Mawasiliano ya karibuni yamekuja wakati Kremlin ikiashiria iko wazi kwa mazungumzo.

Msemaji Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kwamba Rais wa Russia Vladimir Putin alikuwa alikuwa wazi kwa mashauriano tangu “mwanzoni kabisa.”

Putin “alijaribu kuanzisha mazungumzo na wote NATO na Marekani hata kabla ya kuanzisha operesheni maalum ya kijeshi,” Peskov aliongeza, akitumia msingi wa Russia kwa vita nchini Ukraine.

Mapema Ijumaa, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alionekana kuongeza matumaini ya mazungumzo, akisema Putin hivi sasa anaonekana kuwa “amelainika zaidi na yuko wazi kwa mashauriano.”

Maafisa wa Marekani na NATO wamerejea kusema kwamba njia ya haraka kwa Putin kumaliza vita hivi ni kwa majeshi ya Russia kuondoka Ukraine, kitu ambacho kiongozi wa Russia amekataa kutekeleza.

Maafisa wa Magharibi hali kadhalika walisema misingi ya suluhu yoyote lazima ikubaliwe na Ukraine, ambayo imeapa kuyakomboa maeneo yote ambayo hivi sasa yanakaliwa kimabavu na Russia, ikiwemo Crimea, ambayo ilitekwa na Russia mwaka 2014.

Licha ya ya Russia kubadilika, Moscow imeendelea kukataa kufanya mashauriano juu ya kuirejesha mikoa minne ya Ukraine ambayo ilijiingiza mwezi uliopita.

Ukrainian President Volodymyr Zelenskyy has also ruled out any talks with Moscow as long as Putin remains in power.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy pia amefuta uwezekano wowote wa mazungumzo na Moscow wakati ambapo Putin bado yuko madarakani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Ijumaa kuwa hakuna dalili yoyote kwamba Putin anataka kujihusisha kufikia suluhu ya kidiplomasia.

Amesema katika mkutano wa waandishi wa habari Washington akiwa na mwenzake wa Ufaransa, Catherine Colonna, “kila dalili inaonyesha, yuko mbali na nia ya kujihusisha kufikia suluhu ya kidiplomasia, Rais Putin anaendelea kushinikiza kuelekea upande tofauti.”

Baadhi ya taarifa hizi zimetokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG