Akiongea na wanachama wa chama chake cha AK katika bunge, Erdogan alisema Putin alisema Ulaya inaweza kupata gesi yake kutokea nchini Uturuki.
Putin wiki iliyopita alipendekeza Uturuki kuwa ni kituo cha usambazji gesi baada ya mabomba ya Nord Stream kwenye bahari ya Baltic kuahribiwa na milipuko mwezi uliopita.
Umoja wa Ulaya, ambayo awali iliigeukia Russia kwa kiasi cha asilimia 40 ya mahitaji yake ya gesi, hata hivyo inatafuta njia nyingine ili kuondoa utegemezi wa gesi kutoka Russia kufuatia uvamizi wa Putin nchini Ukraine mwezi Februari.
Waagizaji wakubwa wa gesi huko EU kama Ujerumani na Italy wamepata njia mbadala na kuweka akiba ya gesi kabla ya majira ya baridi ambayo huenda yakawa ya hali ngumu zaidi kwasababu ya kupanda kwa bei za nishati na khofu ya mgao wa umeme.
Bomba la Nord Stream 2, lilikuwa linaunganisha Russia na Ujerumani, liliharibiwa mwezi uliopita na kiwango kikubwa cha gesi kuvuja.