Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 25, 2024 Local time: 11:24

Waendesha mashtaka wa Marekani wawashtaki raia watano wa Russia


Jengo la Mahakama ya Marekani.
Jengo la Mahakama ya Marekani.

Waendesha mashtaka wa Marekani Jumatano waliwashtaki raia watano wa Russia kwa kukwepa vikwazo na mashtaka mengine kwa kusafirisha teknolojia za kijeshi.

Teknolojia hizo zilinunuliwa kutoka kwa watengenezaji wa Marekani hadi kwa wanunuzi wa Russia, ambazo baadhi yake ziliishia kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine.

Waendesha mashtaka wa serikali kuu huko Brooklyn walisema vifaa vya kielektroniki vilivyonunuliwa na raia wa Russia Yury Orekhov na Svetlana Kuzur-gasheva ni pamoja na vifaa vya umeme, rada na satelaiti. Baadhi ya vifaa vya elektroniki vilivyopatikana kupitia mpango huo vimepatikana katika majukwaa ya silaha ya Russia yaliyokamatwa nchini Ukraine, waendesha mashtaka walisema.

Walitumia kampuni ya Ujerumani kusafirisha teknolojia za kijeshi, pamoja na mafuta ya Venezuela, kwa wanunuzi wa Russia, waendesha mashtaka walisema.

Orekhov alikamatwa nchini Ujerumani siku ya Jumatatu. Mrussia mwingine aliyeshtakiwa katika kesi hiyo, Artem Uss, amekamatwa nchini Italia na Marekani inataka arejeshwe, waendesha mashtaka walisema. Reuters haikuweza mara moja kumpata mshtakiwa yeyote ili kutoa maoni yake.

XS
SM
MD
LG