Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:32

Uingereza kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi


Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame huko London, tarehe 4 Mei 2023 Picha na Daniel LEAL / AFP.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame huko London, tarehe 4 Mei 2023 Picha na Daniel LEAL / AFP.

Mpango wa Uingereza wa kuwapeleka nchini Rwanda waomba hifadhi utagharimu dola 215,035 kwa kila mtu, kulingana na tathmini ya kwanza ya kina ya ahadi ya serikali katika kukabiliana na idadi kubwa ya watu wanaowasili na boti ndogo ndogo nchini humo.

Serikali ya kiconservative ya Waziri Mkuu Rishi Sunak inataka kuwapeleka maelfu ya wahamiaji zaidi ya kilomita 6,400 nchini Rwanda kama sehemu ya makubaliano na nchi hiyo ya Afrika ya kati yaliyofanyika mwaka jana.

Serikali inauona mpango huo kama msingi wa kuzuia watu wanaoomba hifadhi, wanaowasili na boti ndogo ndogo wakitokea Ufaransa. Sunak analichukua suala hili kuwa moja ya masuala matano anayoyapa kipaumbele huhu kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wabunge wa chama chake cha Conservative na umma kutatua suala hilo, wakati chama hicho kikiwa nyuma ya chama kikuu cha upinzani cha Labour katika kura za maoni kabla ya uchaguzi wa kitaifa utakaofanyika mwakani.

Katika tathmini ya athari za kiuchumi iliyochapishwa Jumatatu, serikali ilisema gharama ya kumpeleka kila mtu nchini Rwanda itajumuisha gharama kama vile malipo ya wastani wa dola 133,485 kwa Rwanda kwa ajili ya kumpokea kila anayeomba hifadhi, dola 28,000 kwa ajili ya ndege na kusindikizwa, na dola 22,882 kwa ajili ya mchakato na gharama za kisheria.

Waziri wa Mambo ya Ndani Suella Braverman alisema gharama hizi lazima zizingatiwe pamoja na athari za kuwazuia wengine wanaojaribu kuingia Uingereza na kupanda kwa gharama za makazi kwa wanaoomba hifadhi.

Iwapo hatua hazitachukuliwa, Braverman alisema kuwa gharama za wanaoomba hifadhi ya makazi zitapanda hadi kufikia dola bilioni 13.9 kwa mwaka, kutoka takriban dola bilioni 4.5 za hivi sasa.

"Tathmini ya athari za kiuchumi inaonyesha wazi kwamba kukaa kimya hakuta saidia," alisema.

Serikali ilisema uwezekano wa kuokoa pesa "haujulikani kabisa ," lakini ilikadiria kuwa hata ikijaribu kuepuka gharama, mpango huo utazwauia karibu watu wawili kati ya watano wanaowasili kwa boti ndogo.

Mwaka jana, rekodi ya watu 45,000 waliingia nchini Uingereza kwa boti ndogo ndogo waliovuka Channel, wengi wao wakitokea Ufaransa. Mwaka huu, hadi kufikia kipindi hiki zaidi ya watu 11,000 wamewasili.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG