Idara hiyo imesema inaamini mtu huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye alikamatwa Jumatano mjini London, amekuwa akishirikiana na mitandao ya usafirishaji haramu wa watu Afrika Kaskazini, kwa kuandaa boti za kusafirisha wahamiaji na kisha kuwasiliana na washirika wao wahalifu wakati wa kuvuka bahari hiyo.
“Tunashuku kuwa mtu huyu amekuwa akiendesha operesheni zake kutoka Uingereza, na kusimamia usafirishaji haramu wa maelfu ya wahamiaji,” Darren Barr, afisa mkuu wa uchunguzi katika idara ya NCA amesema katika taarifa.
NCA ambayo imekuwa ikishirikiana na kikosi cha ulinzi wa pwani cha Italy kama sehemu ya uchunguzi wake, ilitaja tukio la kuvuka bahari mwezi Oktoba mwaka jana ambapo zaidi ya wahamiaji 640 waliokolewa na maafisa wa Italy baada ya kujaribu kuvuka bahari ndani ya boti ya mbao kutoka Libya.
Forum