Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:19

Uganda: Mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine akamatwa baada ya kurejea nchini


Mwanasiasa wa Uganda Bobi Wine.
Mwanasiasa wa Uganda Bobi Wine.

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine alikamatwa Alhamisi aliporejea nchini kutoka safari ya nje, kwa mujibu wa chama chake cha National Unity Platform (NUP).

Mwimbaji huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa aliwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe, Alhamisi asubuhi, baada ya kuzuru nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini.

"Rais wetu alichukuliwa na maafisa wa serikali mara tu alipotua kwenye uwanja wa ndege," David Lewis Rubongoya, katibu mkuu wa NUP, alisema kwenye X, mtandao wa kijamii ambao awali ulijulikana kama Twitter.

Ujumbe huo uliambatana na picha iliyoonyesha wanaume wawili wakimkamata, wakiwa barabarani.

Hakukuwa na kauli ya haraka ya polisi. Wafuasi wa Bobi Wine walikuwa wamepanga kuandamana naye kwa wingi hadi nyumbani kwake kaskazini mwa mji mkuu, Kampala, kumkaribisha, lakini polisi walisema mikusanyiko kama hiyo haikuwa halali.

"Maandamano kama haya yanaweza kutatiza mtiririko wa kawaida wa magari, shughuli za watu binafsi, na zile za biashara kwenye barabara kuu ya Entebbe - Gayaza.

Yanaweza pia kuvutia vitendo vya uhalifu, kuhatarisha watazamaji, madereva wa magari, abiria na biashara kupitia vitendo vya wizi au vitendo vingine vya uhalifu,” msemaji wa polisi wa Kampala Patrick Onyango alisema.

Mwezi uliopita, polisi wa Uganda walitangaza kupigwa marufuku kwa mikutano inayoandaliwa na NUP kote nchini kwa sababu za usalama wa umma.

Forum

XS
SM
MD
LG