Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:54

Uganda: Wabunge wanaomuunga mkono Bobi Wine waachiliwa kwa dhamana


Mwanasiasa wa upinzani wa Uganda, Bobi Wine
Mwanasiasa wa upinzani wa Uganda, Bobi Wine

Wabunge wawili wanaomuunga mkono mwanamuziki maarufu wa Uganda ambaye baadaye aliingia katika siasa Bobi Wine, ambaye pia ni mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni, wameachiwa kwa dhamana  Jumatatu  baada ya kifungo cha  cha miezi  17 jela.

Wabunge hao walikuwa wamefungwa kwa tuhuma za makosa ya mauaji ambayo wapinzani wanadai yalikuwa na ushawishi wa kisiasa.

Wabunge wote wawili, Muhammad Ssegirinya na Allan Ssewanyana, ni wanachama wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Wine, ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa Museveni wakati wa uchaguzi uliopita wa mwaka 2021.


“Wamepewa dhamana, kwa sasa tunashughulikia masharti ya dhamana yao ili waachiliwe," Erias Lukwago, mmoja wa mawakili aliliambia shirika la habari la Reuters.

Walipewa dhamana kabla ya kesi yoyote kwa masharti kwamba wanasalimisha hati zao za kusafiria mahakamani na kulipa takriban dola 5,470 kila mmoja, alisema wakili huyo.

Wabunge hao wawili walishtakiwa kwa tuhuma za mauaji mwezi Septemba 2021, kufuatia matukio ya mauaji ya watu 26 katikati mwa Uganda ambako ni ngome ya upinzani.

Tangu walipo kamatwa mara kadhaa walinyimwa dhamana, mwendesha mashitaka alizuia ombi lao katika misingi kuwa wangeingilia kati uchunguzi wa mauaji hayo. Hakuna tarehe iliyotajwa ya kusikiliza kesi yoyote

Chanzo cha habari hii inatoka shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG