Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:30

Ufaransa na mataifa mengine yenye nguvu waendelea kuwaondoa watu Sudan

Raia wa Ufaransa na wa nchi nyingine wakishuka katika kituo cha kijeshi cha Ufaransa huko Djibouti Apr. 23, 2023.( Picha na Jonathan Sarago/French Ministry of Europe and Foreign Affairs /AFP)
Raia wa Ufaransa na wa nchi nyingine wakishuka katika kituo cha kijeshi cha Ufaransa huko Djibouti Apr. 23, 2023.( Picha na Jonathan Sarago/French Ministry of Europe and Foreign Affairs /AFP)

Mataifa yenye nguvu yameendelea kuwaondoa watu zaidi kutoka Sudan katika operesheni kubwa ya kimataifa.

Hatua hii imechukuliwa baada ya kuzuka kwa mapigano ambayo yamepelekea raia wengi wa kigeni na wa Sudan kukimbia wakihofia usalama wao.

Meli ya kivita ya Ufaransa iliyobeba mamia ya watu walioondolewa ilitia nanga Jumatano asubuhi huko Jeddah , Saudi Arabia.

Hii ni sehemu ya juhudi pana zinazohusisha meli kadhaa za kivita pamoja na usafiri wa ndege.

Ufaransa imetoa mchango mkubwa kupata njia ya kuwaondoa watu wengi kutoka kambi ya jeshi la anga nje ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Raia wa Ufaransa na wa nchi nyingine wakiwasili Djibouti kutoka Khartoum, Aprili 23, 2023. (Photo by ADJ Laure-Anne MAUCORPS ep DERRI / Etat Major des Armées / AFP)
Raia wa Ufaransa na wa nchi nyingine wakiwasili Djibouti kutoka Khartoum, Aprili 23, 2023. (Photo by ADJ Laure-Anne MAUCORPS ep DERRI / Etat Major des Armées / AFP)

Msemaji wa jeshi kanali Pierre Gaudilliare alisema Ufaransa iliwaokoa zaidi ya raia 500 kutoka mataifa 40 kwa kutumia ndege mwishoni mwa wiki baada ya kupata kituo cha anga kaskazini mwa Khartoum Jumamosi.

XS
SM
MD
LG