Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:52

Uchumi wa Afrika kusini umekuwa kidogo licha ya matatizo ya umeme


Wafanyakazi wa kampuni ya umeme ya Eskom wakifanya marekebisho katika kituo cha umeme cha Kusile, tarehe 22 Mei 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP.
Wafanyakazi wa kampuni ya umeme ya Eskom wakifanya marekebisho katika kituo cha umeme cha Kusile, tarehe 22 Mei 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP.

Uchumi wa Afrika Kusini ulikuwa kwa kiwango kidogo katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2023, na kusababisha hofu ya kushuka kwa uchumi wa nchi hiyo yenye maendeleo makubwa ya viwanda barani Afrika.

Idara ya takwimu ya taifa, Stats SA, ileleza Jumanne zinaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari mpaka Marchi, Mapato Jumla ya Uzalishani (GDP) yaliongezeka kwa asilimia 0.4, baada ya kupungua kwa asilimia 1.1 mnamo miezi mitatu ya mwisho ya mwaka jana.

Ukuaji huo umetokea licha ya upungufu mkubwa wa umeme ambao unaendelea kuzorotesha shughuli za kiuchumi, na kukua zaidi ya matarajio ya wachumi wengi.

"Sekta za viwanda na fedha ndio sekta kuu zilizochochea ukuaji katika upande wa usafirishaji wa bidhaa katika uchumi," Stats SA ilisema katika taarifa.

Mteja analinganisha bei katika duka la Pick and Pay huko East London.
Mteja analinganisha bei katika duka la Pick and Pay huko East London.

Wachumi wa benki ya FNB walisema walitarajia "kudorora kidogo kwa uchumi", huku wengine walitabiri kusita kwa ukuaji wa takriban asilimia sifuri.

Afrika Kusini imekumbwa na rekodi ya ugavi wa umeme katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kutokana na matatizo makubwa ya shirika la umeme la Eskom.

Ugavi huo wa umeme umesababisha hasara ya zaidi ya dola milioni 50 kwa siku, kulingana na makadirio ya waziri wa nishati, Mapato ya Uzalishaji kwa ujumla yamekuwa yakiyumba sana kutokana na hali hiyo.

Uchumi wa Afrika Kusini ulipungua kwa asilimia 0.8 katika robo ya pili ya mwaka 2022, baada ya kupanuka kwa asilimia 1.8 katika robo iliyofuata -- kabla ya kudidimia tena katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ya mwaka, kulingana na data iliyofanyiwa marekebisho.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG