Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Malawi Ken Zikhale Ng'oma alisema Kigali iliwasilisha ombi rasmi la kutaka kusaidiwa kuwasaka washukiwa "wababe wa vita”.
"Serikali ya Rwanda imeomba msaada kutoka serikali ya Malawi katika kuwatambua washukiwa 55 ambao kwa sasa wamejifika nchini Malawi. Watu hawa wanajulikana kama wababe wa vita," Ng'oma aliuambia mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika mji mkuu Lilongwe.
Washukiwa wanaodaiwa kujificha nchini Malawi wanasakwa kuhusiana na "vifo vya zaidi ya watu 2,000 vilivyotokea katika baadhi ya makanisa," alisema Ng'oma bila kutoa maelezo zaidi.
Ombi la Rwanda limetolewa wiki kadhaa baada ya kukamatwa kwa Fulgence Kayishema huko Afrika ya Kusini baada ya kuwa mafichoni kwa zaidi ya miongo miwili. Kayishema ni miongoni mwa watoro wanne waliokuwa wakitafutwa na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kutokana na kuhusika kwao katika mauaji ya halaiki.
Kayishema, ambaye alitumia majina mengi ya bandia na nyaraka za uongo, anadhaniwa amekuwa akisafiria na pasipoti ya Malawi.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP
Forum