Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:10

Kipindupindu chasababisha vifo vya watu 10 Afrika Kusini


Wagonjwa wa kipindupindu wapokea matibabu.
Wagonjwa wa kipindupindu wapokea matibabu.

Idara ya afya katika jimbo la Afrika Kusini la Gauteng Jumapili ilitangaza visa vipya 19 vya Kipindupindu ikiwa ni pamoja na vifo 10, katika mji wa Hamman-skraal.  

Afrika Kusini iliripoti kifo chake cha kwanza kutokana na kipindupindu mwezi Februari mwaka huu baada ya wagonjwa waliokuwa na virusi hivyo, kuwasili kutoka nchini Malawi.

Haikubainika wazi ni wagonjwa wangapi wa kipindupindu walioko nchini kote lakini jimbo hilo lenye watu wengi zaidi la Gauteng, ambako Johannesburg na Pretoria zinapatikana, ndilo lililoathirika zaidi.

Kipindupindu kinaweza kusababisha hali mbaya ya kuharisha, kutapika na udhaifu, na huenezwa zaidi kupitia chakula au maji machafu. Ugonjwa huo unaweza kuua ndani ya saa chache, ikiwa hautatibiwa.

Mlipuko wa mwisho nchini Afrika Kusini ulishuhudiwa kati ya mwaka 2008 na 2009, wakati ambapo, takriban visa 12,000 viliripotiwa, kufuatia mlipuko katika nchi jirani ya Zimbabwe.

Hali hiyo inaelezwa kusababisha ongezeko la wagonjwa waliokuwa wametoka nchi za nje, na maambukizi ya ndani.

XS
SM
MD
LG