Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 15:21

Uchaguzi Nigeria: Tume yasimamisha uchaguzi Enugu, hofu za ghasia zatawala


Maafisa wa jeshi la kupambana na ghasia nchini Nigeria wakiwa kwenye mstari kabla ya mkutano wa kampeni wa Chama cha Labour kwenye Uwanja wa Adamasingba ulioko katika jiji la Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, tarehe 23 Novemba 2022. Picha na PIUS UTOMI EKPEI / AFP.
Maafisa wa jeshi la kupambana na ghasia nchini Nigeria wakiwa kwenye mstari kabla ya mkutano wa kampeni wa Chama cha Labour kwenye Uwanja wa Adamasingba ulioko katika jiji la Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria, tarehe 23 Novemba 2022. Picha na PIUS UTOMI EKPEI / AFP.

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imesimamisha uchaguzi wa seneti katika jimbo la kusini mashariki la Enugu, ambako mgombea wa chama cha upinzani cha Labour aliuwawa, Mwenyekiti wa tume hiyo Mahmood Yakubu amesema Ijumaa.

Polisi wamesema mgombea mmoja wa chama cha upinzani na dereva wa basi dogo la kampeni linalomilikiwa na chama kingine waliuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyo ratibiwa katika Jimbo la Enugu siku ya Alhamisi, kabla ya uchaguzi wa Jumamosi.

“Hakutakuwa na uchaguzi wa seneti huko Enugu katika wilaya ya mashariki” Yakubu alisema katika mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na waandishi wa habari, Ni mkutano wa mwisho wa tume hiyo kabla ya uchaguzi wa Jumamosi.

Mamlaka nchini Nigeria zimeanza kupeleka vifaa nyeti vya kupigia kura chini ya ulinzi mkali wenye silaha kwenda kwenye vituo mbalimabli vya upigaji kura nchini humo wakati wanajeshi wakifanya doria katika majimbo yenye ushindani mkali kabla ya uchaguzi mkuu.

Ukosefu wa usalama ulioenea umekuwa wasiwasi mkubwa kwa wapiga kura ambao watawachagua wabunge wapya na rais ambaye atachukua nafasi ya Muhammadu Buhari, ambaye haruhusiwi kugombea tena baada ya kuhudumu kwa miaka minane..

Katika jimbo la kaskazini la Kano, mji mkuu wa kibiashara wa Lagos na jimbo la kusini mashariki la Anambra, ambayo yamegubikwa na wanaotaka kujitenga na ghasia za magenge, wanajeshi wako mitaani chini ya saa 24 kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa.

Katika mji mkuu wa jimbo la Anambra, Awka, maafisa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wamekuwa wakipeleka kwenye vituo karatasi za kura, mashine za kupigia kura na majenereta yanayotumia petroli chini ya ulinzi wa jeshi.

Chanzo cha habari ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG