Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:12

Nigeria kupiga kura; Je mizozo ya kiuchumi na kiusalama itaathiri maamuzi ya wapiga kura?


Mwanamke mkongwe Mnigeria akishiriki katika uchaguzi huko Daura, Nigeria, Machi 28, 2015. Picha na AP Photo/Ben Curtis.
Mwanamke mkongwe Mnigeria akishiriki katika uchaguzi huko Daura, Nigeria, Machi 28, 2015. Picha na AP Photo/Ben Curtis.

Taifa la Nigeria ambalo lina watu wengi zaidi barani Afrika, siku ya Jumamosi wananchi watapiga kura kumchagua rais mpya huku kukiwa na hali mbaya na ukosefu wa usalama na matatizo ya kiuchumi.

Mivutano juu ya uhaba wa fedha taslimu na mafuta ya petroli huenda pia ikawashawishi watu katika upigaji kura wao.

Kinyang’anyiro cha urais kina ushindani mkali sana haukuwahi kutokea kwa karibu miaka 24.

Taifa hilo likiwa na rekodi ya wanigeria milioni 93.4 waliojiandikisha kupiga kura wakiwemo wapiga kura wapya milioni 10, vijana wengi, wachambuzi wanasema mwenendo wa ushindani huu huenda ukawa tofauti kuliko chaguzi zilizopita.
Wakusanyaji maoni wanabashiri kuwa Peter Obi atanufaika sana kutokana na wapiga kura wapya.

Watalaamu wanasema yenye ni nguvu kubwa ya chama cha tatu katika nchi ambako uchaguzi wa rais kwa kawaida umekuwa ni ushindani wa vyama viwili vikuu.

Jason Onwe mfuasi wa mgombea Peter Obi anasema, “mtu huyu namuita ni ubao usio na dosari. Alisema kama una shutuma zozote zilete nizione, na mpaka hivi hakuna mtu hata mmoja hajawasilisha shutuma zozote. Ndiyo maana nitampigia kura Peter Obi.”

Obi ameahidi mageuzi ya kiuchumi na matumizi ya busara katika serikali, lakini anashindana dhidi ya wakongwe katika siasa za Nigeria

Bola Ahmed Tinubu wa chama tawala cha APC, anajulikana kama mwanasiasa mahiri, ameahidi kupambana na ukosefu wa usalama na kuendeleza sera za rais anayeondoka madarakani Muhammadu Buhari.

Pia kuna mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha People’s Democratic. Atiku Abubakar, ambaye ni makamu rais wa zamani. Wafuasi wake wanasema ujuzi wake unamfanya kuwa chaguo zuri.

Nigeria imekuwa ikijitahidi kudhibiti kusambaa kwa ukosefu wa usalama na kuzuia uchumi wa nchi kuanguka.

Lakini watalaamu wanasema hivyo siyo vigezo pekee ambavyo vinawashawishi wapiga kura wakati huu.

Idayat Hassan ni mkurugenzi katika Kituo cha Demokrasia na Maendeleo anasema. “Mchanganyiko wa uhaba wa mafuta katika taifa ambalo linazalisha mafuta kama Nigeria na uhaba wa Naira hivi sasa ndiyo vinafafanua mfumo mzima wa uchaguzi, hata jinsi watu watakavyopiga kura na kitu gani tutarajie kukiona siku ya uchaguzi ambao una ushindani wa karibu sana ambako mambo madogo kwa hakika ndiyo yanahusika,” anasema Idayat.

Benki Kuu ya Nigeria inatekeleza mageuzi ya sarafu ambayo imepelekea uhaba wa fedha taslimu.

Wagombea wengi wameitaka CBN kuongeza tarehe yake ya mwisho ya mpito wa kubadilisha sarafu lakini Benki Kuu, ikiungwa mkono na rais imekataa.

Aliyu Abdullahi ni mkazi wa Abuja ambaye anasema anajitahidi kukabiliana na sera ya fedha na kuongezea kuwa kiasi cha siku tatu zilizopita, vurugu kuhusu fedha taslimu ni suala ambalo limepelekea ghasia katika maeneo yake na watu wawili waliuawa.

Katika kuelekea siku ya upigaji kura, hata hivyo wafanyakazi wa uchaguzi wameshambuliwa katika maeneo kadhaa. Huku mamilioni ya watu wataekelea kwenye vituo vya kupigia kura, huko kuna wasi wasi wa uwezekano wa ghasia.

XS
SM
MD
LG