Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:35

Timu ya kandanda ya wanawake ya Nigeria bado inapigania haki ya malipo sawa


Timu ya kandanda ya wanawake ya Nigeria Super Falcons.
Timu ya kandanda ya wanawake ya Nigeria Super Falcons.

Timu ya kandanda ya wanawake ya Nigeria Super Falcons  hivi sasa iko nchini Australia kushiriki michuano ya FIFA 2023 ya kombe la Dunia kwa wanawake. 

Wachezaji hawa wanawake walioko barani Afrika, ni kama wale ambao wako hapa nchini Marekani, ambao mara kwa mara wanalipwa kiwango cha chini kuliko wenzao wanaume.

Timu ya taifa ya Nigeria, ikiwa imeshinda mataji tisa kati ya 11 barani humo. Timu hii inaliwakilisha bara la Afrika katika mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa wanawake inayofanyika nchini Australia na New Zealand.

Blessing Emmanuel alianza kucheza soka wakati alipokuwa na umri wa miaka 12. Lakini familia yake awali haikutaka acheze na ilijaribu kumalizimisha aache kucheza kandanda.

“Baba yangu alikuwa akisema, ‘hapana, sidhani nataka mtoto wangu wa kike awe katikati ya wavulana’, vitu kama hivyo. Ilibidi nimshawishi sana,” anasema Emmanuel.

Alifanikiwa. Mwaka 2020, Emmanuel alijiunga na Klabu ya Mpita ya Naija Ratels, na mwaka jana, aliongoza timu ya taifa ya Nigeria ya vijana chini ya miaka 17 kwenda India na timu hiyo ilishinda medali ya shaba.

Kocha wa Naija Ratels, Sunny Udu, anasema kuwa lengo la awali la klabu lilikuwa kuwasaidia wasichana walio katika mazingira duni.

Sunny Udu anasema “Si kila msichana ambaye ana fursa kwa vile anatoka kwenye nyumba nzuri. Utagundua kwamba wengi wao, wako mitaani wanafanya kile ambacho hawataki kukifanya, ili tu w

Timu ya kandanda ya wanawake Super Falcons ya Nigeria.
Timu ya kandanda ya wanawake Super Falcons ya Nigeria.

aweze kukidhi baadhi ya majukumu yao.”

Soka la wanawake linazidi kuongezeka umaarufu barani Afrika na timu ya taifa ya Nigeria, Super Falcons, ni miongoni mwa timu zinazofanya vizuri.

Ni timu pekee ya kiafrika kushiriki katika mashindano ya kombe la dunia la FIFA mwaka 1991 na hivi sasa iko nchini Australia kushiriki katika mashindano ya FIFA ya 2023 ambayo yanaanza hivi leo.

Licha ya mafanikio, wachezaji wanawake wanasema mara kwa mara hawalipwi vizuri ukilinganisha na wenzao wanaume na wamekuwa siku zote wakidai kulipwa sawa.

Wiki iliyopita, gazeti la Daily Mail la Uingereza liliripoti kuwa wachezaji wa Nigeria huenda wakasusia mechi yao ya kwanza dhidi ya Canada iliyopangwa kuchezwa kesho July 21 wakipinga kutolipwa bonasi zao. Bunmi Oladeji ni mchezaji wa Super Falcons.

“Kuwa msichana mdogo, matarajio ya wazazi wako ni kwa wewe kufanya kazi, kuolewa na halafu unaanza kupata watoto, lakini wewe, una hamu kubwa ya kucheza soka, huku ndiko ninakotaka kutengeneza pesa,” anasema Bunmi Oladeji.

Mashabiki wana wasi wasi mizozo huenda ikapunguza ari kwenye mashindano hayo, lakini Shirikisho la Kandanda Nigeria limeahidi kulishughulikia suala hilo. Kocha msaidizi wa Super Falcons, Sunny Udu, anadhani usawa utatokea.

Udu anaongezea “Wanataka kuona wanaume wanalipwa kiasi na wanawake wanalipwa, lakini itachukua muda.”

Mwezi Machi, FIFA, taasisi ambayo inasimamia uratibu wa soka kote duniani, ilitangaza kwamba kila mchezaji katika Kombe la Dunia la Wanawake, watapewa dola 30,000. Wachezaji wa timu itakayoshinda kila mmoja atapewa dola 270,000.

Hiyo inafanya safari ya Super Falcons iwe na tija – lakini bado inawaacha wakijitahidi kupambana kupata kulipwa huko nyumbani.

Forum

XS
SM
MD
LG