Biden, na marais wa zamani Bill Clinton na Barack Obama wameka ujumbe katika Twitter wakiomboleza kifo cha Pele
Wapenzi wa soka barani Afrika nao wameungana na wenzao duniani kuomboleza kifo cha mchezaji wa Brazil Pele siku ya Ijumaa.
Mjini Abuja, Nigeria, wapenzi wa kandanda wamemtaja Pele alikuwa “mkubwa sana kuliko mchezo wenyewe,” na alikuwa kama kiongozi wa dunia… ni shujaa wa aina yake,” alisema mtaalam wa Masuala ya Utawala.
Mtaalam huyo Perez Ayoola wakati akisoma vichwa vya habari vya magazeti alisema: “Alikuwa kama kiongozi wa dunia kwa sababu alijitoa ... kama mtoto alikupa matumaini. Unajua namna alivyoanza kucheza mpira bila ya kuvaa viatu na baadaye kuiwezesha Brazil kuingia katika michuano ya kombe la dunia na kuifanyia nchi yake mambo mengi sana. Kipindi hicho alikuwa ni hazina kwa nchi yake.
Mjini Johannesburg, mashabiki wa kandanda walisema ilikuwa ni siku ya masikitiko kwa soka. "Ni siku ya masikitiko ametutoka. Unafahamu, tutamkumbuka sana, na masikitiko kwa mchezo wa kandanda, alikuwa na jukumu kubwa katika michezo:” alisema shabiki wa kandanda Daniel Norman.
“Nadhani katika enzi yake, alikuwa hodari, unajua, kama tulivyokuwa tunasema, unapokua, mchezaji pekee wa soka ambaye umemfahamu na kumsikia, inapokuja kandanda, alikuwa ni Pele, na unajua wengi walitaka kumuiga, kila mtu alitaka kuwa kama yeye. Kama ulicheza soka. Unajua, tutamkumbuka sana, na inasikitisha sana, alikuwa na jukumu kubwa katika michezo, na hajawahi kuchezza nje ya nchi yake, nadhani hakutaka kwenda kucheza Ulaya, na kwa kweli aliotuonyesha huna haja ya kwenda popote, kama unaweza kucheza soka ndani ya nchi yako na unaweza kuwa mchezaji mkubwa sana,” aliongezea Norman.
Mashabiki wa soka nchini Kenya siku ya Ijumaa waliomboleza na kifo cha mkongwe wa soka wa Brazil Pele. Katika mitaa yenye harakati nyingi katika jiji la Nairobi, Frederick Ochieng ameiambia Reuters alikuwa amevutiwa na Mbrazil huyo tangu utoto wake.
"Bwana huyo alikuwa shujaa, nilikuwa nampenda tangu nilivyokuwa mdogo, nilikuwa nataka niwe kama yeye lakini hilo halikuwa,” alisema.
Pele, alifariki mjini Sao Paulo Alhamisi (Desemba 29). Alikuwa ni mtu pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu kama mchezaji, na katika uchezaji wake wa miaka 21 alifunga jumla ya magoli 1,283.
Pele aliitembelea Kenya mwaka 1976 na kutoa mafunzo kwa vijana wa nchi hiyo waliyokuwa wananyanyukia katika soka kuwa tegemeo la taifa.
Mkazi wa Nairobi Christopher Mburu alisema “tumempoteza nyota wetu.”