Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:20

Mfalme wa soka duniani Pele afariki dunia


Nyota wa zamani wa kandanda wa Brazil hayati Pele enzi za uhai wake. Desemba 1, 2017. (Picha ya AP)
Nyota wa zamani wa kandanda wa Brazil hayati Pele enzi za uhai wake. Desemba 1, 2017. (Picha ya AP)

Pele, mchezaji mashuhuri wa soka wa Brazil aliyeondoka kwenye umaskini wa kutembea peku peku hadi kuwa mmoja wa wanasoka wakubwa na wanaojulikana sana katika historia, alifariki dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 82.

Pele, mchezaji mashuhuri wa soka wa Brazil aliyeondoka kwenye umaskini wa kutembea bila ya viatu hadi kuwa mmoja wa wanasoka wakubwa na mashuhuri wanaojulikana sana katika historia, alifariki dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 82.

Kifo cha mwanasoka huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa mchezaji kilithibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye Instagram.

Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi.

Aliibeba Brazil hadi kwenye kilele cha soka na kuwa balozi wa kimataifa wa mchezo huo katika safari iliyoanzia mitaa ya jimbo la Sao Paulo, ambapo alicheza mpira wa kutengenezwa na soksi iliyojaa magazeti au matambara.

Gwiji huyo wa Brazil, ambaye jina lake halisi lilikuwa Edson Arantes do Nascimento, aliisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia mwaka wa 1958, 1962 na 1970 na anabakia kuwa kinara wa ufungaji wa timu ya taifa akiwa amefunga mabao 77 katika mechi 92.

Nyota wa sasa wa Brazil, Neymar, alifikisha magoli hayo kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu nchini Qatar, akifunga bao lake la 77 katika michezo 124.

Pele alikuwa mfungaji mdogo zaidi wa Kombe la Dunia mwaka 1958 alipofunga bao dhidi ya Wales akiwa na umri wa miaka 17 tu mashindano hayo yalipofanyika Stockholm, Sweden. Rekodi yake bado ipo, na hadi sasa, bado ndiye mchezaji pekee chini ya miaka 18 kufunga bao katika Kombe la Dunia.

XS
SM
MD
LG