Ushindi katika mechi hiyo ya ufunguzi, mechi ya kwanza ya timu hiyo kwenye hafla ya kuonyesha soka la kimataifa, utaipa Qatar pointi muhimu na kasi inayohitajika ili kutinga hatua ya 16 bora, alisema fowadi wa zamani wa Qatar Mohamed Mubarak al-Mohannadi.
Natazamia washinde mchezo wa kwanza. Ni muhimu zaidi...Hatuwaombi washinde Kombe la Dunia, aliongeza.
Wengi katika timu ya Qatar inayoshiriki Kombe la Dunia ambao wengi wao ni raia na wahamiaji waliozaliwa hapa, waliokulia na kupewa uraia nchini Qatar walitafutwa wakiwa watoto na waliibukia kutoka kwenye Chuo cha Aspire cha dola bilioni 1.3.
Sheikh Jassim Bin Hamad Al-Thani, ndugu yake mfalme wa Qatar, alianzisha Aspire mwaka 2004 ili kuendeleza wachezaji wa ndani miaka sita kabla ya timu ya taifa ya Qatar kufuzu moja kwa moja kushirikia katika Kombe la Dunia la 2022 ilipotangazwa mwenyeji wa fainali hizo.
Wengi katika timu hiyo ikiwa ni pamoja na nyota wawili Akram Afif na mfungaji bora Almoez Ali wamekuwa wakicheza pamoja chini ya kocha mzawa wa Uhispania, Felix Sanchez tangu mwaka 2014, alipoiongoza kama timu ya umri wa chini ya miaka 19 ya Qatar hadi taji la ubingwa wa vijana la AFC.
Wengi wa wachezaji hawa wamekuwa na Sanchez tangu wakiwa watoto ni kama baba kwa hawa watu, alisema Mohamed El Gharbawy, mwandishi wa habari wa soka mwenye makazi yake Qatar.
Nchini Qatar, Sanchez anasifiwa kwa kuingiza mtindo wa Kihispania wa "mguso mmoja, pasi ndogo, kazi nzuri ya pamoja, uchezaji wa kumiliki mpira" alisema Ahmed Hashim, mhariri wa Qatar Football Live, chaneli ya Twitter.
Tangu Juni, Sanchez amewapeleka wachezaji wa Qatar katika kambi za mazoezi nchini Uhispania na Austria
Walicheza mfululizo wa mechi za kirafiki mwezi Septemba, na kupoteza dhidi ya Canada na Croatia chini ya umri wa miaka 23 na kutoka sare na Chile na, katika wiki za karibuni, walishinda mechi za kirafiki dhidi ya Nicaragua, Guatemala na Honduras.
Uchezaji mseto huo unaonyesha kuwa taifa hilo la Ghuba ya Kiarabu si timu ya kutisha huenda timu hiyo isipate nafasi dhidi ya wapinzani wao wengine wa Kundi A katika Kombe la Dunia Senegal na Uholanzi.
Lakini timu ya hiyo ya Qatari imewahi kushangaza siku za nyuma, maarufu zaidi iliposhinda Kombe la Asia mnamo 2019 baada ya ushindi wa 3-1 wa fainali dhidi ya Japan na kuwacharaza wenyeji wa michuano hiyo Umoja wa Falme za Kiarabu 4-0 katika nusu-fainali.
Sanchez tangu wakati huo amefanya mabadiliko machache katika timu yake ya kwanza.
"Baadhi wanaweza kusema kuendelea kunasaidia. Wengine wanaweza kusema kwamba kama tungekuwa na nafasi za wazi kwa ushindani, hiyo ingeongeza kiwango cha uchezaji na motisha kwa wachezaji," Hashim alisema.
"Hatutaweza kujua kama hilo ni jambo zuri au baya hadi baada ya Kombe la Dunia.” alisema.