Ecuador waliwashinda Qatar kwa mchuano wa kwanza kombe la dunia 2022, kwa mabao mawili kwa sufuri Jumapili, ambayo yalipachikwa na mshambuliaji mkongwe Enner Valencia, katika siku ambayo hafla ya ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ya mwezi mmoja ilifanyika.