Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:51

Tanzania yaadhimisha Siku ya Wazee Duniani


Wazee wahudhuria sherehe za kuadhimisha siku yao Tanzania
Wazee wahudhuria sherehe za kuadhimisha siku yao Tanzania

Tanzania iliadhimisha Siku ya Wazee Duniani huku ikikadiriwa kuwa taifa hilo lina takriban wazee milioni 3 sawa na asili mia 5.6 ya watu wote. 

Wakati wa hafla iliyofanyika Jumamosi, serikali ilitakiwa kuwasaidia watu wa umri mkubwa pale inapohitajika kwa manufaa ya jamii, huku walio wengi wakikabiliwa na Changamoto mbalimbali za kimatibabu.

Waswahili wanasema Uzee ni dawa lakini pamoja na umaarufu wa Msemo huo, bado wazee mbalimbali kutoka katika taifa hilo la Afrika Mashariki wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za matibabu hasa kutokana na kunyemelewa na maradhi mbalimbali yasiyoambukiza.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:42 0:00

Mzee Twalihata Mdhihiri kutoka Bagamoyo amelalamikia tabia ya wahudumu wa zahanati za Afya kutothamini kadi za wazee za matibabu huku akiishauri Serikali iachane na mfumo uliopo wa kutumia kadi ili waweze kupewa bima ya Afya.

Inafahamika Wazee ni watu muhimu ambao wengi wametulea lakini kutokana na kasi ya maisha na siku kwenda kwa haraka umri wao sasa umesogea hali inayolazimu taifa kuwatazama

Diwani wa Kata ya Mindu kutoka katika Manispaa ya Morogoro Zuberi Mkalaboko ameishauri Serikali kubadilisha mfumo wa upatikanaji wa huduma ya wazee uliopo huku akiishauri Serikali ijikite katika kuwapatia wazee bima ya afya ya Daraja la juu

Kwa upande wake Mzee Pashua Shekue amesema namna nzuri ya kuwafurahisha wazee katika kuadhimisha siku yao ni kuyafanyia kazi mambo yanayozungumzwa katika siku hiyo.

Aidha Mzee Shekue amesema wazee wengi wanachukuliwa kama tabaka lilotengwa hivyo ameitaka Serikali ya Tanzania katika kuwatunza wazee wasiiishie katika huduma za matibabu tu bali hata katika kujua makazi yao, vyakula vyao na kuwasaidia vipato kama ilivyo kwa mataifa mengine

Siku ya Wazee Duniani huadhimishwa tarehe Mosi Oktoba ya kila mwaka ambayo ilitengwa mwaka 1990 baada ya mkutano mkuu wa umoja wa mataifa kuamua rasmi kuanzisha siku hii.

Nchini Tanzania idadi ya wazee inatajwa kuwa kubwa zaidi kuliko watoto chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa takwimu za karibuni, kufikia mwaka 2050 karibu asilimia 21 ya watu wote duniani watakuwa ni wazee.

Imetayarishwa na Amri Ramdhani, Sauti ya Amerika, Dar es Salaam.

XS
SM
MD
LG