Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:38

Benki kuu ya Tanzania yachukua hatua kupunguza mfumuko wa bei

Jengo la benki kuu ya Tanzania.
Jengo la benki kuu ya Tanzania.

Benki kuu ya Tanzania itapunguza mzunguko wa fedha katika uchumi mwezi Septemba na Oktoba ili kupunguza kasi ya mfumuko wa bei katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, taarifa ya kamati ya sera ya fedha ya benki hiyo (MPC) iliyochapishwa Jumamosi ilieleza.

Taarifa inaeleza kwamba “Katika muktadha wa mfumuko wa bei na bei za bidhaa, ambazo zimechangia kuongezeka kwa shinikizo la mfumuko wa bei nchini, MPC iliidhinisha benki hiyo kuendelea na kupunguza taratibu mzunguko wa fedha Septemba na Oktoba 2022.

Uamuzi huo wa sera unalenga kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei, huku ikilinda shughuli za kiuchumi.

Mfumuko wa bei nchini Tanzania ulipanda hadi asilimia 4.6 mwezi Agosti kutoka asilimia 4.5 mwezi uliopita, huku uchumi wa nchi ukikabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo ukuaji dhaifu wa dunia, bei za juu za bidhaa, hali mbaya ya kifedha na kuzuka upya kwa COVID-19 katika baadhi ya nchi taarifa hiyo iliongeza.

XS
SM
MD
LG