Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:23

Tanzania : Polisi bado wanaendelea na uchunguzi juu ya madai ya kushambuliwa Mbowe


Freeman Mbowe
Freeman Mbowe

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema linaendelea kufanya upelelezi kuhusu tukio la mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, Freeman Mbowe kudai ameshambuliwa na watu wasiojulikana alipokuwa akirejea nyumbani kwake wakati wa usiku.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto katika taarifa yake kwa vyombo vya habari nchini humo amesema taarifa walizonazo ni kutoka kwa muathirika Mbowe alidai kuwa alipokuwa akiingia nyumbani kwake akiwa anatokea kwa mzazi mwenzake Joyce Mkuya mbunge wa viti maalum Chadema alishambuliwa na kuumizwa mguu.

Mbowe alidai kuwa alipiga kelele wakati anashambuliwa lakini hakupata msaada wowote isipokuwa kutoka kwa dereva wake ambaye alimchukua na kwenda naye hadi kwa mbunge Mkuya na kisha kuelekea hospitali kwa matibabu na kuongezea hakuna umuhimu wa kutoa taarifa polisi kabla ya kwenda kwa Joyce na hospitali.

Kwa mujibu wa kamanda wa mkoa wamepata ushahidi wa kutosha kutoka kwenye eneo la tukio unaoonyesha walikuwepo watu ambao wangeweza kuona shambulizi hilo.

Muroto amesema kuwa polisi walipofika nyumbani kwa Mbowe walimkuta kijana wake James Mbowe ambaye 'hakufahamu kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani na badala waliona ni vyema kumjulisha Joyce Mkuya aliyekuwa mbali na eneo la tukio.'

Uchunguzi kwa mujibu wa polisi umethibitisha kuwa siku ya tukio Mbowe alitembelea maeneo kadhaa ya starehe ambayo yaliuza vileo ikiwepo Royal Village na kupata vinywaji. Kwa mujibu wa taarifa ya polisi alipofika hospitali alionekana akiwa katika hali ya "ulevi chakari" kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.

Muroto amesema bado idara ya polisi inaendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa tukio hilo na kuwasihi wananchi wote wenye taarifa zinazoweza kusaidia katika upelelezi kuwasiliana na polisi.

XS
SM
MD
LG