Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:45

Taasisi ya ICG yaonya kutokea mzozo wa muda mrefu Somalia


Rais Mohamed Abdullahi Farmajo
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo

Taasisi ya kimataifa ya kushughulikia mizozo, International Crisis Group, ICG imeonya Jumamosi kwamba mzozo wa kisiasa wa muda mrefu nchini Somalia unaigia katika awamu mpya.

Taasisi hiyo pia imetahadharisha kuwepo hatari ya mvutano mkubwa kati ya wanaoumunga mkono Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kama Farmajo na wanaompinga.

Onyo hilo limetolewa siku moja baada ya mapambano kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la kamanda wa zamani wa polisi wa Mogadishu aliyefukuzwa baada ya kupinga hatua ya rais kuongeza muda wa muhula wake madarakani.

ICG inaeleza mapambano hayo yanadhidirisha mgawanyiko ndani ya vikosi vya usalama vya Somalia unaotishia kuzuka mapigano kati yao na hapo kutoa nafasi kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabab kutumia fursa hiyo kuimarisha nguvu zao.

Ripoti hiyo inaendelea kueleza kwamba, hali ya Somalia ni mbaya kutokana na habari kwamba upinzani unatafakari juu ya kuunda serikali yao, mgawanyiko katika vyombo vya usalama na upinzani kuongezeka dhidi ya rais aliyekuwa madarakani baada ya kuongeza muda wa utawala wake.

XS
SM
MD
LG