Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:43

Kenya Airways yarejesha safari za ndege kila siku kuelekea New York


Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya Airways
Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya Airways

Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) limeanzisha tena safari zake za kila siku kwenda New York wakati  ikitumia fursa ya ongezeko la mahitaji ya safari za ndege katika njia hiyo.

Shirika hilo liliongeza idadi ya safari zake katika njia hiyo mpaka mara tano kwa wiki kutoka safari tatu Desemba mwaka 2021, likielezea kiwango kikubwa cha wasafiri.

Mahitaji ya juu ni ishara nzuri kwa sekta ya utalii, ambapo Marekani bado ni chanzo kikubwa sana cha soko la nje ya nchi huku ikichangia asilimia 16 ya wageni 870,465 walioingia nchini humo mwaka 2021.

Shirika hilo la ndege pia limeongeza idadi ya safari zake kuelekea miji kama Paris kutoka safari tano kwa wiki hadi safari za kila siku, Madagascar safari tisa kwa wiki kutoka safari saba, Comoros imeongeza safari tano kutoka nne, Amsterdam imeongeza safari tano kutoka nne kila wiki.

KQ inaendelea inakabiliana na mahitaji yanayo badilika ya safari za kuelekea Marekani tangu kuanza kwa janga la Covid -19, na hivyo kubadilisha idadi ya safari zaz ndege kuelekea huko.

“Uboreshaji wa mtandao ni hatua ya kawaida na imefahamika kwa kurejea safari za ndege wakati sekta ya usafiri wa anga ikipata nafuu kutokana na janga la Covid-19 na katika kuisaidia sekta ya utalii nchini Kenya,” limeeleza shirika hilo la ndege.

Shirika la ndege la Kenya lilianzisha safari za moja kwa moja kuelekea uwanja wa kimataifa wa JF Kennedy huko New York kutoka uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) mjini Nairobi mwezi Oktoba 2018, huku ikionekana kuwa safari za Marekani ndiyo msingi wa shirika hilo kupata mafanikio.

Hata hivyo shirika hilo limekuwa likihangaika kutokana na kuwepo safari chache kuelekea Marekani tangu iliporejesha huduma zake kufuatia miezi kadhaa ya kusitisha safari hizo kutokana na hali ya janga la Covid -19.

Safari za ndege zitaliwezesha shirika hilo kunufaika kutokana na wasafiri wanaounganisha safari zao kupitia JKIA kutoka miji mikuu ya nchi nyingine za Afrika ambazo hazina usafiri wa moja kwa moja kwenda katika nchi yenye uchumi mkubwa kabisa duniani.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la “The East African” linalochapishwa Kenya

XS
SM
MD
LG