Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:33

Serikali ya mpito Libya yamuachilia mtoto wa Ghadhafi


Saadi Gadhafi, mtoto wa Moammar Gadhafi, alipokuwa mahakamani mjini Tripoli, Libya, Feb. 7, 2016.
Saadi Gadhafi, mtoto wa Moammar Gadhafi, alipokuwa mahakamani mjini Tripoli, Libya, Feb. 7, 2016.

Saadi Gadhafi, mtoto wa kiume wa diktekta wa zamani wa Libya, marehemu Moamar Ghadhafi, ambaye alipinduliwa na kuuawa katika ghasia za mwaka 2011, ameachiliwa kutoka jela, kulingana na serikali ya mpito.

Saadi, mtoto wa tatu, hivi sasa ana umri wa miaka 47 alijulikana kwa maisha yake alikuwa mpenda starehe na mcheza soka wa kulipwa nchini Italy.

Saadi Moamar Gadhafi ameachiliwa kutoka gerezani kufuatia uamuzi wa mahakama miaka kadhaa iliyopita, chanzo cha wizara ya sheria kilisema Jumapili, bila kusema ikiwa bado yupo nchini humo.

Saadi Gadhafi alikabidhiwa kwa familia yake, kulingana na taratibu za kisheria, serikali ya umoja wa kitaifa ilithibitisha katika taarifa.

Ripoti kadhaa za vyombo vya habari, zilidokeza kuwa Gadhafi tayari aliondoka kwa ndege kuelekea Uturuki.

Chanzo kingine ambacho kinafanya kazi kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka kilithibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba Ghadhafi alikuwa ameachiliwa.

XS
SM
MD
LG