Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:26

Benki kuu ya Libya kuimarishwa


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh

Benki kuu ya Libya ambayo kwa muda mrefu imegawanyika katika matawi mawili  kutokana na mapigano, Alhamisi imefanya ukaguzi wa hesabu za kitaifa uliosuburiwa kwa muda mrefu

Hatua hiyo inaonekana kuwa muhimu kwelekea kuunganisha taasisi za taifa hilo. Benki hiyo inayodhibiti hesabu za mapato ya mafuta kwenye taifa hilo la Afrika kaskazini iligawanyika mwaka 2014 kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoigawa nchi mara mbili.

Mwaka uliopita hata kabla ya sitisho la mapigano kufikiwa, kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya kimataifa ya Deloitte ilikagua hesabu za matawi yote mawaili ya benki hiyo kuelekea kuunganisha taifa chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa.

Hapo Alhamisi balozi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jan Kubic aliwasilisha waraka huo mbele ya kaimu waziri mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibah , kwenye sherehe zilizofanyikia Tripoli.

Miongoni mwa viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na mkuu wa benki kuu ya Libya Seddik al Kebir na mwenzake anayesimamia tawi la mashariki lililojitenga Ali al Hebri.

XS
SM
MD
LG